Uchambuzi wa Riwaya ya <em>Kiu</em> Kwa Kutumia Nadharia ya Saikolojia Changanuzi

Article

Uchambuzi wa Riwaya ya Kiu Kwa Kutumia Nadharia ya Saikolojia Changanuzi

DOI: 10.1080/23277408.2018.1540127
Author(s): Saade Said Mbarouk Chuo Kikuu cha Abdulrahma Al-Sumait, Zanzibar

Abstract

Makala haya yanaonesha nadharia ya Saikolojia Changanuzi na namna inavyotumika katika uchambuzi wa riwaya ya Kiu. Makala itachunguza kwa makini mbinu za kisaikolojia za wahusika kama, uzungumzi nafsi, daiolojia ya ndani na ndoto ambavyo vinaonesha hali zao za ndani na namna wahusika hao wanavyotumia uhusika wao kuibua dhamira mbalimbali katika riwaya hiyo. Pia makala itaangalia mbinu za uwasilishaji wa mawazo na usimulizi zinavyoweza kutumika katika kumuangalia mwandishi namna ung’amuzibwete (unconsciousness) na mtazamo wake kuhusu maisha na matendo katika jamii yake. Vilevile itamuangalia msomaji na mhakiki anavyoweza kuathirika na matini aliyoisoma. Mawazo hayo wanaelezwa kwa kutumia hali ya kimaadili na mitazamo ya maisha yanayotokana na matendo ya kinafsi.

Get new issue alerts for Eastern African Literary and Cultural Studies