Utendajipepe wa Fasihi Simulizi: Haja ya Kuwa na Tawi Jipya

Article

Utendajipepe wa Fasihi Simulizi: Haja ya Kuwa na Tawi Jipya

DOI: 10.1080/23277408.2019.1685583
Author(s): Angelus Mnenuka University of Dar es Salaam, Tanzania

Abstract

Makala hii inajadili dhana ya utendaji wa fasihi simulizi mtandaoni. Kiini cha makala hii ni hoja kuwa uainishaji wa fasihi hivi sasa, yaani fasihi simulizi na fasihi andishi, umekitwa katika aina za uwasilishaji, ambazo ni uwasilishaji wa kimazungumzo na wa kimaandishi. Ugunduzi wa intaneti, na kuingia kwa teknolojia hiyo katika vifaabebe kama vile simu na sleti kwa kutumia programu mbalimbali za kuwasiliana, umewezesha mawasiliano ya kimaandishi ya papo kwa papo au yasiyo ya papo kwa papo. Mawasiliano hayo yamechangia kuibuka kwa lugha ya kipekee ambayo sifa zake hazifanani na sifa ya lugha ya kimazungumzo wala lugha ya kimaandishi. Licha ya kuwa na lugha ya kipekee, baadhi ya tanzu za fasihi simulizi, kwa namna ya kipekee, zimekuwa zikitendeka mtandaoni kwa kutumia lugha hiyohiyo. Utafiti huu umefanyika kwa kutumia Nadharia ya Utendaji bila kuathiri nafasi na umuhimu wa matini katika kazi za kifasihi. Data za utendaji wa vitendawili mitandaoni zilikusanywa, zilichambuliwa, na matokeo yake yanawasilishwa katika makala hii. Kwa kutumia utendaji wa vitendawili vya Kiswahili mtandaoni, ninapendekeza liundwe tawi jipya la fasihi ambalo litafumbata sifa za aina hiyo ya mawasiliano.

Get new issue alerts for Eastern African Literary and Cultural Studies