Nomino Na Majina Ya Pekee Katika Fasihi Tafsiri: Yatafsiriwe Au La?

Article

Nomino Na Majina Ya Pekee Katika Fasihi Tafsiri: Yatafsiriwe Au La?

DOI: 10.1080/23277408.2019.1593088
Author(s): Nahashon A. Nyangeri Department of Kiswahili, University of Nairobi, Kenya , Rachel Wangari Modern languages, St Lawrence University, USA

Abstract

Nomino au majina ya pekee ni mojawapo ya maswala muhimu anayokumbana nayo mtafsiri katika mchakato wa tafsiri yoyote iwayo. Mara nyingi mtafsiri hutanzika iwapo majina hayo yanafaa kufasiriwa au la. Nomino za pekee katika fasihi mara nyingi huwa ni malighafi anayoyatumia mwandishi kuwaumba wahusika wake kwa namna ya kuwafanya viumbe wa kuaminika katika ulimwengu wa fasihi pamoja na kuwa mojawapo ya vyanzo vya kuupata ujumbe wakati wa kusoma matini. Hivyo basi, yanapojitokeza kwenye matini za kifasihi, huwa mojawapo ya mambo anayokumbana nayo mtafsiri wa kazi za kifasihi. Majina haya huibua changamoto kubwa kwa mtafsiri. Hali hii huwa ngumu zaidi kwa kuwa majina haya huweza kudokeza habari kuhusu jinsia, umri, asili ya mtu, usuli, maana mahususi, utajiri wa lugha na wa kitamaduni. Mara nyingi yanachukuliwa hivihivi katika tafsiri kwa msingi kwamba hayatafsiriki na wala hayafai kutafsiriwa. Hata hivyo, wapo wataalamu wengine ambao hushikilia kwamba majina ya pekee yana maana fulani, hivyo basi yanahitaji kutafsiriwa, lakini kimkakati.

Get new issue alerts for Eastern African Literary and Cultural Studies